Wednesday, August 4, 2010

LIL KIM KUTUA BONGO



HII NI HISTORIA FUPI YA MWANADADA LIL KIM AMBAYE ATAKAMUA SIKU YA JUMAMOSI PALE LEADERS KWENYE TAMASHA FIESTA
KIMBERLY DENISE JONES,QUEEN BEE a.k.a.LIL KIM alizaliwa BROOKLYN,MAREKANI ,mwaka 1975 tarehe 11 JULY na hivi sasa ana umri wa miaka(35)lil kim ni mtunzi na ni mwimbaji wa muziki aina ya HIP HOP,pia ni ACTRESS ambaye alikuwa ni member wa JUNIOR M.AF.I.A….Lili kim kaishi maisha ya kitaa kwa muda mrefu mara baada ya Baba na mama yake kutengana akiwa na umri wa miaka tisa then after NATORIOUS B.I.G. ndipo alipomsaidia…
Alianza mziki mwaka 1996 na albamu yake ya kwanza iliitwa CONSPIRACY ambayo ilifanya vyema katika chati za muziki mwaka 1996 alitoa tena albamu nyingine iliyopewa jina la HARD CORE..ambayo ilikuwa na vibao viwili hatari kama vile ‘NO TIME’ na ‘CRUSH ON YOU’..Hapo alikaa kwa muda mrefu kidogo takribani miaka minne mpaka mwaka 2000 akatoa albamu nyingine iliyoitwa THE NOTORIOUS K.I.M na 2003 akatoa nyingine iliyoitwa LA BELLA MAFIA ambazo zote zilikuwa ziko kwenye CHAT….
Mwaka 2005 mdada huyu alihukumiwa kwenda jela kosa la kuidanganya mahakama kwa kesi iliyokuwa ikimuandama rafiki yake ambaye alikuwa akihusishwa na mauaji..lil kim ana albamu nyingine nyingi kama vileTHE NAKED TRUTH,DANCING WITH STARS..
Ukiondoa maisha yake aliyopitia lili kim ameshafanya na wanamuziki wakubwa duniani akiwemo BAD PRESIDENT wa sasa PUFF DADDY,MISSY ELLIOT,ANGIE MARTINEZ,DA BRAT,TLC enzi hizo na wanamuziki wengine kibao kesha act movie akishirikiana na MARTIN LAWRENCE movie hiyo inaitwa ‘NOTHING TO LOSE’ ambayo ilikuwa nominated katika tuzo za GRAMMY AWARD Yeye mwenyewe kim ana tuzo kibao za BET AWARDS
LIL KIM bado anatamba na kibao chake kikali kinachoitwa ‘lighters up’ ambayo ilikuwa namba moja katika kituo maarufu kilichopo huko marekani kupitia kipindi cha 106&park kwa muda wa wiki mbili mfululizo na top ten za bilboard ngoma hiyo pia ina tamba kule germany,uk, na huko finland

1 comment: